Wakulima wa maua nchini Kenya wameeleza matumaini yao wakati soko la maua la Ulaya likianza kufunguka taratibu baada ya kufungwa kwa wiki kadhaa kutokana na janga la virusi vya Corona.
Wakulima hao wamesema walikuwa na wasiwasi kutokana na wimbi la pili la kuvurugika kwa soko licha ya soko hilo kuanza kufunguliwa hatua kwa hatua. Pia wamesema, kutokana na kupungua kwa soko la maua, mauzo ya kila siku yameshuka kwa asilimia 80, na kuathiriki kwa kiasi kikubwa kipato chao.
Shirikisho la Usafirishaji wa Bidhaa Mbichi la Kenya limesema, ndege za kusafirisha mizigo zimeongeza mara tatu bei ya bidhaa kwa kilo na kufikia dola za kimarekani tatu, na gharama nyingine za ziada ambazo zinapunguza faida kwa wakulima wa maua.
Kenya inasafirisha karibu asilimia 90 ya maua katika nchi za Ulaya, soko ambalo limevurugwa kutokana na hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona, ikiwemo kusitisha safari za ndege za abiria na mizigo, pamoja na kufungwa kwa soko la maua.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |