• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yafuatilia mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii wa China

    (GMT+08:00) 2020-05-21 20:51:09

    Wakati mikutano miwili ya China inapofanyika, nchi mbalimbali za Afrika zinafuatilia mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii wa China katika kipindi kijacho.

    Mkurugenzi wa idara ya Asia na Austrilia katika wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw. Davit Igar amesema mafanikio ya mikutano miwili ya China hasa sera ya maendeleo ya uchumi yana umuhimu mkubwa kwa bara la Afrika. Akisema,

    "Ninafuatilia jinsi China itakavyofufua uchumi na kuurudisha hali ya kawaida, hii ina maana muhimu kwa Afrika. Kama uchumi wa China ukifufuka, shughuli za kiuchumi zitarudishwa na shughuli ya uuzaji bidhaa kwa nchi za nje itarudishwa, jambo litakalozisaidia nchi za Afrika kukabiliana na athari zinazotokana na COVID-19."

    Mkurugenzi wa kituo cha uchunguzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja wa Chuo Kikuu cha Zambia Bw. Sand Enjaland amesema, Zambia pia inafuatilia miswada ya mikutano miwili ya China kuhusu maendeleo ya uchumi ya China. Anasema,

    "Sasa maambukizi ya COVID-19 yamesababisha athari mbaya sana kwa uchumi wa nchi za Afrika, tunatarajia sera ziatakazopangwa kwenye mikutano miwili hiyo ya China sio tu zitasaidia kuhimiza maendeleo ya uchumi wa China, bali pia zitasaidia ushirikiano wa dunia na maendeleo ya uchumi wa dunia, kuzisaidia nchi mbalimbali duniani kushinda vita dhidi ya janga la maambukizi ya virusi vya Corona."

    Aidha, kutokana na janga hilo, sera za kutimiza maendeleo ya amani na kidiplomasia zitakazopangwa kwenye mikutano miwili ya China pia zinafuatiliwa sana na nchi za Afrika.

    Msaidizi wa waziri wa mambo ya Asia wa wizara ya mambo ya nje ya Misri Bw. Hani Salim alisema,

    "Kwanza ninafuatilia jinsi China itakavyoendelea kutimiza maendeleo kwa njia ya amani hasa katika sekta ya uchumi chini ya athari mbaya ya COVID-19 duniani, aidha ninafuatilia jinsi China itakavyopanga sera ya kidiplomasia chini ya hali ya sasa ya kimataifa."

    Naye mkurugenzi wa kituo cha uchunguzi wa China na Afrika cha Chuo Kikuu cha Johannesburg cha Afrika Kusini Bw. David Monyae anasema, "Mikutano hiyo miwili ya China sio tu inahusiana na maslahi ya taifa la China pekee, bali pia inahusiana na pande mbalimbali na utandawazi wa dunia, rais Xi Jinping wa China aliwahi kueleza kuwa kushirikiana kuhimiza utaratibu wa pande nyingi kwa nchi mbalimbali duniani kunasaidia ustawi na utulivu wa uchumi wa dunia."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako