• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kocha Roberto Martinez kuendelea kuwafunda Ubelgiji

  (GMT+08:00) 2020-05-22 08:36:42

  Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez, 46, amesema analenga kuacha "kumbukumbu nzuri" katika ulingo wa soka baada ya kuongeza mkataba wake kambini mwa kikosi hicho hadi mwishoni mwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar. Kocha huyo mzawa wa Uhispania alipokezwa mikoba ya Ubelgiji 2016 na mkataba wake ulikuwa utamatike rasmi mwishoni mwa fainali za Euro 2020 ambazo kwa sasa zimeahirishwa hadi mwaka 2021 kutokana na janga la corona. Chini ya Martinez, Ubelgiji waliambulia nafasi ya tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizoandaliwa nchini Urusi mwaka 2018. Sasa, Ubelgiji wapo kileleni mwa orodha ya viwango bora vya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) na wanajivunia kusajili ushindi katika mechi zote 10 za kufuzu kwa fainali za Euro 2020. Wanapigiwa upatu wa kutawala Kundi B linalowajumuisha pia Denmark, Finland na Urusi na pengine hatimaye kunyanyua ufalme wa fainali zijazo za Euro.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako