• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Tyson Fury atamba kutopigwa hadi kufikia kustaafu kwake

    (GMT+08:00) 2020-05-22 08:37:30

    Bondia Muingereza Tyson Fury amewatumia ujumbe wapinzani wake wanaowaza kupigana naye kwa kutamba kuwa hatapigwa hadi kufikia kustaafu kwake na kwamba hana mpango wa kuachia mikanda aliyonayo ya ubingwa wa uzani wa juu duniani na kila atakaouchukua ataubeba hadi atakapotangaza kustaafu mchezo wa ngumi. Bondia huyu anayesakwa na mabondia tofauti ambao wanamchukulia kama "mti wenye matunda kupigwa mawe" ili kupata wanachokitarajia ndivyo ilivyo kwake, ambapo mabondia Anthony Joshua, Dylian Whyte na Deontay Wilder kwa pamoja wanapiga dua zao za kutosha tu ili wapigane naye. Tyson aliyemvua mkanda bondia aliyekuwa kwenye ubora wake, Wladmir Klitschko kwa pointi mnamo mwaka 2015 na baada ya droo kwenye pambano la kwanza mwaka 2018 dhidi ya Deontay Wilder, alimvua Mmarekani huyo mkanda wa WBC uzani wa juu zaidi uliokuwa unashikiliwa na bondia huyo kwa miaka mitano, mwezi februari mwaka huu katika pambano la pili. Kuna uwezekano mkubwa sana Tyson Fury akarudiana na Deontay Wilder katika pigano la tatu kwa mujibu wa mkataba walioandikishana na tayari Tyson ameshathibitisha kwamba ataanza na Wilder ammalize ndipo atapigana na Anthony Joshua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako