• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: David Mwantika wa Azam FC asema amepata ofa kucheza Saudi Arabia

  (GMT+08:00) 2020-05-22 08:37:52

  Beki wa Azam FC David Mwantika amesema mara baada ya kumalizana na uongozi wa klabu hiyo sasa anafikiria kuanza maisha mapya nje ya Tanzania. Mwantika ambaye bado yupo katika utata wa kuachana na klabu hiyo amesema anaendelea kupokea ofa mbalimbali za kucheza soka nje ya Tanzania. Beki huyo wa zamani wa Prisons amesema mara baada ya kumalizana na Azam FC tayari ameshapokea ofa nzuri ya kwenda kucheza Soka Saudi Arabia. Hata hivyo amesema bado wanapambana na Azam hawataki kumuachia na wanataka kumtoa kwa mkopo kwa klabu ambayo hajakubaliana nayo lakini yeye anasema hataki kuondoka vibaya na kuonelea ni bora waachane kwa amani kila mmoja akafanye lake kwani kuna kesho pia. Utata wa Mwantika na Azam FC ulianza siku chache kabla ya kufungwa kwa usajili wa dirisha dogo wakati Azam wakimtaka kwenda Lipuli kwa mkopo hatua ambayo aligomea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako