• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi Kuu Tanzania kurejea Juni Mosi

  (GMT+08:00) 2020-05-22 08:38:19

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa masuala ya michezo ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara ni ruksa kuanza ifikapo Juni Mosi 2020. Magufuli amesema sasa michezo ni ruhusa kuendelea kuanzia Juni Mosi ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara, daraja la Kwanza na mingine. Pia michezo ya majeshi na mambo ya sanaa. Hata hivyo suala la mashabiki uwanjani ameliacha kwa Wizara ya Afya. JPM amessema hali ya maambukizi imepungua na wagonjwa hospitalini wamepungua na hivyo kuamua kuruhusu michezo. Masuala yote ya mijumuiko isiyo ya lazima ilisimamishwa Machi 17 kutokana na Janga la Virusi vya Corona ambapo kwa sasa Serikali imesema kuwa hali ni shwari nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako