Taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, imesema raia 119 wa Tanzania waliokwama nchini Umoja wa Falme za Kiarabu UAE kufuatia mlipuko wa COVID-19, wamerudishwa nyumbani jana Alhamisi.
Taarifa hiyo inasema raia hao wa Tanzania walikwama nchini UAE kwa miezi mitatu baada ya safari za ndege za kimataifa kusitishwa kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona kote duniani. Wiki iliyopita, raia 246 wa Tanzania waliokwama nchini India kutokana na janga hilo pia walirudishwa nyumbani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |