Wizara ya kilimo ya Kenya jana Alhamisi ilizindua kanuni mpya kusaidia kuongeza tija kwenye sekta ya chai, kuinua ufanisi katika mnyororo wa thamani na kuweka uwazi kwenye sekta hiyo.
Waziri wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika nchini Kenya Bw. Peter Munya amesema kanuni mpya zinahitaji viwanda vyote vya chai kujiandikisha kwa serikali na waandaaji wa mnada ili kushiriki kwenye mnada wa chai moja kwa moja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |