Takwimu zilizotolewa jana na Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) zinaonyesha kuwa, idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika imezidi elfu 95.
Taarifa iliyotolewa na kituo hicho imeonyesha kuwa katika saa 24 zilizopita idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona katika bara la Afrika imeongezeka kwa watu 3,603 na kufikia 95,201 kwa ujumla, na idadi ya vifo imeongezeka kwa watu 85 na kufikia 2,997 kwa ujumla. Wakati huohuo wagonjwa takriban 2,267 wamepata nafuu katika saa 24 zilizopita.
Kituo cha Africa CDC kimeongeza kuwa hadi sasa virusi vya Corona vimesambaa kwenye nchi 54 za Afrika, na Afrika Kusini, Misri, Algeria na Morocco ni nchi zilizoathiriwa zaidi barani humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |