• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu wa China wabadilishana uzoefu na madaktari wa Msumbiji kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-05-22 09:32:29

  Madaktari wa uzazi na wa watoto wa China wamebadilishana uzoefu na wenzao wa Msumbiji kuhusu kinga na tiba ya virusi vya Corona kwa wanawake wajawazito na watoto kwenye mkutano uliofanyika kwa njia ya video katika Hospitali Kuu ya Maputo (HCM).

  Kwenye mkutano huo wataalamu kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Sichuan, walizungumzia kinga na tiba ya virusi vya Corona kwa watoto walioambukizwa virusi hivyo, na usimamizi juu ya kipindi muhimu cha ujauzito kwa wanawake wakati wa janga hili.

  Mkuu wa Hospitali ya HCM Mouzinho Saide, amesema mfululizo wa mafunzo yameleta matokeo mazuri yaliyowawezesha madaktari wa hospitali hiyo kuboresha kazi yao katika tiba na usimamizi wa wagonjwa wakati wa janga hili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako