Benki ya Dunia imesema imepitisha mkopo wa dola milioni 43 za kimarekani kwa ajili ya Kenya ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na tishio linalotokana na uvamizi wa nzige wa jangwani na kuimarisha mfumo wa serikali ya nchi hiyo wa kujiandaa kukabiliana na janga hilo.
Mkurugenzi wa nchi wa Benki hiyo nchini Kenya Bw. Felipe Jaramillo, amesema uvamizi wa nzige unaweza kuhatarisha usalama wa chakula baadaye mwaka huu na kuna uwezekano bei za chakula zikaongezeka kama hakutakuwa na uingiliaji wa haraka.
Bw. Jaramillo ametoa taarifa ikisema benki hiyo inashirikiana na wenzi wengine wa maendeleo, ili kurejesha na kuimarisha maisha ya wakulima, wafugaji na familia zenye hali duni kiuchumi ambazo zimeathiriwa na janga hilo na kukabiliwa na hali ya kukosekana kwa usalama wa chakula.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |