• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Magufuli wa Tanzania aruhusu vyuo, michezo kuanza tena

  (GMT+08:00) 2020-05-22 10:04:09

  Rais John Magufuli wa Tanzania ametangaza kuwa vyuo vikuu nchini humo vitafunguliwa tena tarehe mosi mwezi Juni baada ya kupungua kwa idadi ya maambukizi ya COVID-19, na kuziagiza wizara ya elimu na wizara ya fedha na mipango kufanya maandalizi ya kufungua tena vyuo vikuu.

  Aidha ametangaza kuanza tena kwa mashindano ya michezo kuanzia tarehe mosi mwezi Juni, ili kusaidia katika mapambano dhidi ya COVID-19, akizitaka wizara zinazohusika kufanya maandalizi, na safari za ndege za kimataifa zitaanza tena tarehe 27 mwezi Mei, na kuongeza kuwa watalii wanaotembelea nchi hiyo hawatawekwa karantini.

  Baada ya hayo bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ya Tanzania (HESLB) imetangaza kuwa imeidhinisha mkopo wa elimu shilingi bilioni 63.7 (karibu milioni 27.5 za dola za kimarekani) kwa ajili ya chakula na malazi kwa wanafunzi kufuatia tangazo la Rais John Magufuli la kufunguliwa tena kwa vyuo vikuu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako