• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Trump asema Marekani haitaweza zuio kama kukiwa na wimbi la pili la virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-05-22 10:12:50

  Rais Donald Trump wa Marekani amesema Marekani haitafunga uchumi kama kukiwa na wimbi la pili la virusi vya Corona.

  Alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu wasiwasi wa kuwepo kwa wimbi la pili la virusi vya Corona alipokuwa kwenye ziara katika kiwanda cha magari cha Ford, rais Trump amesema kuweka zuio la kudumu si mkakati mzuri kwa jimbo au nchi. Kuweka zuio bila ukomo kutaleta janga la afya ya umma. Ili kulinda afya ya wananchi, ni lazima Marekani ihakikishe uchumi wake unafanya kazi.

  Majimbo 50 nchini Marekani yametangaza mipango ya kuanza kulegeza zuio dhidi ya virusi vya Corona, na kufungua tena uchumi. Wataalamu wa afya wameonya kuwa huenda wimbi la pili la virusi vya Corona litatokea kwenye majira ya mpukutiko na baridi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako