• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasema itajitoa kwenye Mkataba wa Anga huru

    (GMT+08:00) 2020-05-22 10:13:16

    Serikali ya Marekani imetangaza nia ya kujitoa kwenye Mkataba wa Anga huru.

    Kwa mujibu wa kanuni za kujitoa kwenye mkataba huo, Marekani itajitoa rasmi kwenye mkataba huo baada ya miezi sita.

    Mkataba huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2002, unaruhusu ndege za uchunguzi zisizo na silaha za nchi zilizosaini mkataba huo kuruka kwenye anga ya nchi nyingine mwanachama kama hatua za kujenga uaminifu.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Russia Bi. Maria Zakharova, amesema Russia inasubiri Marekani kufafanua kujitoa kwenye Mkataba wa Anga huru.

    Bi. Zakharova amesema Russia bado haijapokea taarifa rasmi au ufafanuzi kutoka Marekani. Mkataba huo wa kimataifa una muundo wa utekelezaji, na umeweka majukumu yaliyothibitishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako