Rais wa Tanzania John Magufuli na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta wamekubaliana kwamba Mawaziri kutoka nchi hizo mbili wanapaswa kukutana ili kusuluhisha mzozo unaoendelea katika mpaka wa nchi hizo mbili juu ya upimaji wa Corona.
Kesi za Corona zikizidi kuongezeka katika mpaka wa Namanga, Kenya imejaribu kuchukua tahadhari kwa kupima dereva yeyote anaye ingia nchini kupitia mpaka wa Namanga.
Na katika vipimo hivyo ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa muda sasa mwanzoni mwa wiki hiii watu 53 wako walipatikana na virusi hivyo na kati yao, 51 ni raia wa Tanzania.
Jambo ambalo lilimlazimu Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kufunga mpaka wa Namanga na vijia vingine vya kuingia na kuondoka Tanzania kufuatia ongezeko la visa vya virusi vya Corona miongoni mwa madereva kutoka nchi hiyo jirani.
Hatua ambayo ili leta kutoelewana kati ya nchi hizo na Tanzania pia kuamua kupiga marufuku malori kutoka Kenya kuingia Tanzania, wakidai madereva wa malori ndio huingiza virusi vya corona nchini humo.
Katika mvutano huo wa kufungwa kwa mpaka wa Namanga, Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza kuwa amefanya mazungumzo na Rais wa Kenya uhuru Kenyatta na wakakubaliana mawaziri husika wa mataifa hayo mawili wasuluhishe mgogoro huo.
Kwani janga la Corona halitasambaratisha uhusiano wa Tanzania na Kenya.
"Nimepigiwa simu na Rais wa Kenya kuhusu migogoro ilipo mpakani, na tumekubaliana mawaziri wetu wa uchukuzi pamoja na wakuu wa mkoa watakutana mpakani wajadili hili suala walimalize, twahitaji biashara wakenya nao wanahitaji biashara huku"
"Huu ni wakati wa kujenga uchumi, Corona haikuanza barani Afrika na kwa hivyo haifai kuwa chanzo cha fitina ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili tusije tukashindwa kufanya biashara kwa sababu ya ugonjwa huu,".
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |