Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Yao Shaojun amezitaka pande mbalimbali za Somalia kushirikiana kwa ajili ya kuhakikisha uchaguzi wa amani na kuhimiza mchakato wa kisiasa.
Amesema Somalia imeingia katika kipindi muhimu, na uchaguzi ni kipaumbele. Ameongeza kuwa rais wa Somalia amesaini mswada wa uchaguzi kuwa sheria, kikosi kazi cha taifa cha usalama wa uchaguzi kimetambua mamlaka yake na kuanza kupitisha mswada wa usalama wa usajili wa wapigakura. Maendeleo hayo yanaonyesha kikamilifu nia thabiti ya Somalia katika kusukuma mbele uchaguzi wa amani.
Amesema China inaunga mkono pande mbalimbali nchini humo kutupia macho maslahi ya kimsingi ya nchi, kuimarisha ushirikiano na mazungumzo, na kushirikiana kuhimiza mchakato wa uchaguzi na wa kisiasa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |