• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Young Africans kuwarudisha Eymael, Riedoh Berdien

  (GMT+08:00) 2020-05-22 16:13:51

  Klabu ya Young Africans imepanga kuwarejesha makocha wa timu hiyo Luc Eymael (Kocha Mkuu) na Riedoh Berdien (Kocha wa Viungo) ambao wapo nje ya nchi baada ya selikali kutangaza kuendelea kwa Ligi kuu kuanzia Juni Mosi. Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa Young Africans Hassan Bumbuli amesema wamepanga kuwatumia tiketi za ndege makocha hao, baada ya Rais Magufuli kutangaza kuwa ndege kutoka mataifa mengine zitaanza kuruhusiwa kutua nchini. Kuhusu Mlinda Mlango Farouk Shikhalo, Bumbuli amesema klabu ya Young Africans itafanya juhudi zote kuhakikisha anarejea kwa wakati licha ya sintofahamu iliyozuka kwenye mipaka ya Kenya na Tanzania. Katika hatua nyingine Bumbuli amesema wachezaji wamepokea kwa furaha taarifa za kurejea tena kwa ligi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako