• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nigeria yaonya matumizi ya hydroxychloroquine kama tiba ya virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-05-22 18:42:15

  Serikali ya Nigeria imeonya dhidi ya matumizi ya dawa za malaria aina ya Hydroxychlroquine kama tiba ya watu wenye maambukizi ya virusi vya Corona, ikisema dawa hiyo haijaidhinishwa kwa matumizi kama hayo.

  Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kupambana na COVID-19 nchini Nigeria Boss Mustapha amesema, onyo hilo limetolewa baada ya kikosi hicho kupokea ripoti kuwa Wanigeria wamenunua kiasi kikubwa cha Hydroxychloroquine ili kutibu virusi vya Corona.

  Amesisitiza tena kuwa dawa hiyo haijaidhinishwa na mamlaka husika za afya na madawa kwa matumizi ya kutibu virusi hivyo nchin Nigeria, na kuongeza kuwa kununua dawa bila ya ushauri wa daktari kunaweza kuongeza hatari ya vifo vinavyoweza kuepukwa.

  Mpaka kufikia jana jioni, Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa nchini Nigeria kiliripoti kesi mpya 339 za virusi vya Corona, na kufanya idadi ya jumla ya watu waliokutwa na maamvukizi ya virusi hivyo kufikia 7,016, huku wengine 211 wakifariki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako