• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Modeli mpya yatabiri rais Trump atashindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu

  (GMT+08:00) 2020-05-22 18:45:36

  Modeli mpya iliyotolewa na kampuni ya ushauri ya Oxford Economics ya Uingereza imetabiri kuwa rais Donald Trump wa Marekani atashindwa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu kutokana na kuzorota vibaya kwa uchumi wa Marekani kufuatia janga la virusi vya Corona.

  Modeli hiyo imefanikiwa kutabiri matokeo ya kila uchaguzi mkuu wa Marekani tangu mwaka 1948 isipokuwa kwa mwaka 1968 na 1976.

  Wakati huohuo, matokeo ya maoni ya kiraia yaliyotolewa na Chuo Kikuu cha Quinnipiac cha Marekani yameonesha kuwa, mgombea wa urais kwa chama cha Democratic Joe Biden alipata kura asilimia 11 zaidi ya rais Trump, ikimaanisha asilimia 50 ya watu watampigia kura Biden na asilimia 39 watampigia kura Trump. Katika utafiti uliofanywa na chuo kikuu hicho mwezi Aprili, pengo la kura kati yao lilikuwa ni asilimia 8, na sasa limeendelea kuongezeka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako