• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina uwezo wa kutimiza malengo ya maendeleo

    (GMT+08:00) 2020-05-22 19:50:34

    Ripoti ya kazi za serikali inayotolewa kila mwaka kwenye mkutano wa Bunge la Umma la China ni kiashiria muhimu cha mwelekeo wa maendeleo ya uchumi na utungaji wa sera. Ripoti ya mwaka huu haikutaja lengo la ukuaji wa uchumi, na imesisitiza kuhakikisha ajira na maisha ya watu, kushinda vita dhidi ya umaskini, na kujitahidi kumaliza ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

    Swali ambalo wengi wanajiuliza ni kwamba, kwa nini mwaka huu ripoti ya kazi za serikali ya China haikuweka lengo la ukuaji wa uchumi? Hivi sasa maambukizi ya virusi vya Corona bado yanaendelea katika nchi mbalimbali, na uchumi wa dunia umedidimia sana. Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limekadiria kuwa mwaka huu, uchumi wa dunia utapungua kwa asilimia 3. Kutokana na utatanishi wa hali ya maambukizi ya virusi hivyo na biashara ya kimataifa, maendeleo ya uchumi wa China yanakabiliwa na changamoto zisizotarajiwa. Hivyo China haiwezi kuweka lengo la ukuaji wa uchumi, bali inatumia nafasi hiyo kutimiza malengo mengine ya maendeleo.

    Ili kutimiza malengo hayo, serikali ya China imepanga kazi sita kuu, ambazo ni kuongeza nguvu katika utekelezaji wa sera ili kuhakikisha ajira, kuchochea nguvu ya soko kwa kusukuma mbele mageuzi ili kuimarisha injini mpya za maendeleo, kupanua mahitaji ya ndani ili kugeuza njia ya maendeleo, kuhakikisha kutimiza lengo la kuondoa umaskini, kuendeleza kilimo na kusaidia wakulima kuongeza kipato, kuinua kiwango cha mageuzi ili kutuliza biashara na uwekezaji wa nje, na kuhimiza mageuzi na maendeleo ya shughuli za kijamii ili kuboresha maisha ya watu. Mpango wa kazi hizo unathibitisha kuwa, China inajitahidi kupiga hatua zaidi wakati inapodumisha utulivu wa maendeleo ya uchumi.

    Maambukizi ya virusi vya Corona yameleta athari kubwa kwa uchumi na jamii ya China, na ili kupunguza athari hiyo, kwenye ripoti yake, serikali ya China imetoa hatua halisi. Kwa mfano, China itaongeza kiwango cha nakisi ya bajeti mpaka asilimia 3.6 ambayo ni kama dola bilioni 140 za kimarekani, na kutoa dhamana ya dola bilioni 140. Wakati huohuo, serikali itasamehe ada na kodi za dola bilioni 350 kwa makampuni, ili kuhakikisha ajira na maisha ya watu.

    Ripoti hiyo inasema, China itafanya kampeni ya kuwasaidia watu maskini kwa njia mbalimbali, ili kutimiza lengo la kuondoa umaskini uliokithiri mwaka huu kama ilivyopanga. Aidha, kwa mujibu wa ripoti hiyo, China itainua kiwango cha kufungua mlango, ili kutuliza biashara na nchi za nje na uwekezaji wa nje. Ahadi hiyo si kama tu ni kwa ajili ya kukabiliana na athari iliyosababishwa na virusi vya Corona kwa biashara kati ya China na nchi za nje, bali pia itasaidia kutuliza mnyororo wa ugavi duniani.

    Kutokana na kuwa na mfumo maalumu wa kisiasa na kijamii, msingi imara wa uchumi na soko kubwa, China yenye watu bilioni 1.4 itashinda changamoto yoyote na kutimiza malengo ya maendeleo ya mwaka huu, na kuendelea kutoa mchango kwa uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako