• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haitakumbwa na mgogoro wa chakula

    (GMT+08:00) 2020-05-22 20:18:04

    Waziri wa kilimo na vijiji wa China Bw. Han Changfu amesema, China haitakumbwa na mgogoro wa chakula.

    Bw. Han amesema, viwango vya kujitegemea vya vyakula muhimu vya China, ikiwemo mpunga na ngano, vimefikia asilimia 100, na akiba ya vyakula hivyo imepita uzalishaji wa mwaka, na kuweza kukidhi mahitaji ya wachina wote kwa mwaka mmoja.

    Bw. Han pia amesema, mavuno ya chakula ya China yameendelea kuwa mazuri kwa zaidi ya miaka 10, na pia China imedumisha uzalishaji wa chakula kwa mwaka zaidi ya tani milioni 650 kwa miaka mitano mfululizo. Kiwango cha chakula kwa kila mtu hapa China kimezidi kigezo kilichotangazwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa. Amesema China imechukua hatua nyingi kuhakikisha uzalishaji wa chakula ili kukabiliana na athari ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Hivi sasa, hali ya kilimo imekuwa nzuri, na kilimo cha majira ya mchipuko kimemalizika kwa asilimia 90, na kilimo cha ngano ya majira ya joto kitakuwa kizuri zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako