• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wenyeji wa mkoa wa Tabora wapongeza serikali kwa kuapata umeme

  (GMT+08:00) 2020-05-22 20:22:15
  Wenyeji wa mkoa wa Tabora wameishukuru serikali kupitia Wizara ya Nishati kwa kuwaunganisha na kuwawashia umeme. Wenyeji hao ambao wengi wao ni kutoka kijiji cha Loya wilayani Uyui wanasema walikuwa wakiona wao kupata umeme ilikuwa ni kama ndoto.

  Walisema hayo baada ya Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, kuwasha umeme katika kijiji hicho na kukagua maendeleo ya usambazaji umeme.

  Walisema, kwa miaka mingi wamekuwa wakipewa ahadi zisizotekelezeka na wakati mwingine wakikatishwa tamaa ya kupata umeme kwa kuwa kijiji hicho kiko umbali mrefu kutoka ilipo miundombinu ya umeme na jiografia isiyo rafiki kufika maeneo hayo.

  Dk. Kalemani kwa upande wake alisema baada ya kusikia malalamiko na kuona uhitaji mkubwa wa umeme kwa kijiji hicho ambacho hakijafikiwa na mradi wa kusambaza umeme (REA) kwa kipindi hiki, aliliagiza Shirika la Umeme nchini humo (Tanesco) kupeleka umeme kwa gharama zao katika kijiji hicho.

  Alisema kijiji cha Loya kina wakulima wengi wa mpunga, karanga na wafanyabiashara ambao wanahitaji huduma ya umeme katika kuendesha shughuli zao za kiuchumi.

  Tanesco ilitenga zaidi ya Sh. bilioni tatu ili kuhakikisha umeme unafika katika kijiji hicho, ambacho kiko umbali mrefu kutoka ilipopita miundombinu ya umeme.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako