• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya Equity yaanza mikakati ya kuwalinda wateja wake

  (GMT+08:00) 2020-05-22 20:22:31
  Benki ya Equity ya Kenya imesema imeweka mikakati ya kuwaokoa wateja ambao wameathiriwa vibaya na janga la Corona ambalo linaendelea kuwakaba koo wafanya biashara wengi hivi sasa. Tangazo hilo limeonekana kukaribishwa na wafanya biashara wengi waliokuwa wamechukua mikopo kutoka kwa benki hiyo. Awali Benki hiyo ilikuwa imetangaza kuwa inalenga kufanyia marekebisho mikopo ya shilingi bilioni 92 kwa ajili ya kuwaokoa wateja wake. Baadhi ya hatua ambazo huenda zikachukuliwa na benki hiyo ni pamoja na kuongeza muda wa kuanza kulipa mkopo wa hadi miaka mitatu hadi janga hili la Corona litakapopungua. Benki ya Equity ni benki ya 6 baada ya benki ya KCB,Absa, Cooperative, NCBA na Stanchart kutangaza msukosuko wa ulipaji mikopo baada ya benki kuu ya Kenya kutangaza sheria za ulipaji mikopo kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona nchini Kenya. Hatua hiyo imepelekea watu wengi kuachishwa kazi, kupungua kwa mapato na hata kuwapa likizo ya lazima baadhi ya wafanya kazi wake.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako