• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viongozi watakiwa kufuata sheria katika kuwatengea ardhi wawekezaji

  (GMT+08:00) 2020-05-22 20:22:48
  Viongozi wa vijiji nchini Tanzania wametakiwa kufuata taratibu za kisheria katika kugawa ardhi kwa wawekezaji ikiwamo kuwashirikisha wananchi badala ya kujiamulia wenyewe ili kuepuka kuibua migogoro kati ya wananchi na wawekezaji.

  Kwa mujibu wa Ofisi ya mkoa wa Mbeya, mkutano mkuu wa Kijiji ndio wenye mamlaka ya kugawa ardhi ya kijiji.

  Ofisi hiyo imesema kazi ya viongozi wa vijiji hasa ofisa mtendaji na mwenyekiti ni kupokea maombi ya wanaotaka kupewa ardhi na kuitisha mikutano ya vijiji ili wananchi wajadili na kuridhia ama kutoridhia kugawa ardhi yao kulingana na uhitaji.

  Kwa mujibu wa sheria ya ardhi, kijiji kinaruhusiwa kugawa ardhi isiyozidi hekta 50 kwa mtu mwingine na kwamba ikizidi ukubwa huo zipo mamlaka zingine ambazo zinahusika na hivyo mhitaji wa ardhi hiyo atatakiwa kuziona.

  Kuhusu mpango wa matumizi bora ya ardhi, kila kijiji kinatakiwa kuwa na matumizi bora ya ardhi kwa maelezo kuwa utaratibu huo unasaidia kuondoa migogoro ya ardhi kwa kuepusha mwingiliano wa shughuli za kibinadamu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako