• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni nyingi zafanya kazi chini ya uwezo wao Kenya

  (GMT+08:00) 2020-05-22 20:23:05

  Kampuni nyingi nchini Kenya zinadaiwa kufanya kazi chini ya uwezo wao kutokana na makali ya janga la corona. Kwa mujibu wa ripoti iliyoandaliwa na kampuni ya KMPG, asilimia 42 ya kampuni za kutengeneza bidhaa zinaendesha shughuli zake chini ya nusu ya uwezo wao huku asilimia 37 ya kampuni ndodo ndogo zomelazimika kufunga kabisa uzalishaji wake.Wakati huo huo asilimia 79 ya kampuni zilizofanyiowa uchunguzi zinaonesha kupungua kwa mapato huku asilimia 86 ya biashara ndogo ndogo zikiwa katika hali hiyo. Hali hiyo imewafanya wafanyabiashara wengi kuwa na wakati mgumu wa kutekeleza majukumu yao ya kifedha.Baadhi ya sekta ambazo zimeathiriwa kabisa ni pamoja na sekta ya nguo, mbao na vifaa vya nyumbani magari. Hata hivyo licha ya msukosuko huo, asilimia 81 ya kampuni za kutengeza bidhaa zimesema hazioni zikifunga biashara zao kutokana na mtikisiko wa janga la corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako