• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Umma la China waonyesha imani ya utawala wa China

  (GMT+08:00) 2020-05-22 20:42:57

  Mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Umma la China umefunguliwa leo mjini Beijing, na kuhudhuriwa na Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China na wa serikali.

  Mkutano huo ambao hufanyika mwezi Machi katika miaka 22 iliyopita, uliahirishwa hadi mwezi Mei kutokana na janga la COVID-19. Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alitoa ripoti ya kazi za serikali katika mwaka uliopita, kutoa mapendekezo ya kazi za mwaka huu, na kuziwasilisha ili kujadiliwa kwenye mkutano huo.

  Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, washiriki wote walikaa kimya kwa dakika moja kuomboleza watu waliofariki kutokana na janga hili.

  Bw. Li amesema, mwaka jana ingawa China ilikabiliwa na changamoto nyingi, imemaliza lengo kuu la mwaka mzima, uchumi wa taifa uliendelea kwa utulivu, maisha ya watu yameboreshwa zaidi na kuweka msingi muhimu wa kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

  "Katika siku za baadaye, ingawa maendeleo ya nchi yetu yanakabiliwana changamoto kubwa, lakini tuna faida ya mfumo maalum wa siasa, msingi imara wa uchumi, uwezo mkubwa wa soko na hekima ya wachina ya kufanya kazi kwa bidii. Tukiwa na ujasiri na imani kukabiliana na changamoto, kuongeza nguvu ya kujiendeleza, kulinda na kutumia vizuri kipindi hiki muhimu cha kimkakati cha kujiendeleza, matatizo yaliyopo bila shaka yatatatuliwa, maendeleo ya China yatakuwa na matumaini mazuri. "

  Bw. Li pia amesema, serikali ya China itaweka kipaumbele katika kuleta utulivu wa soko la ajira na kulinda maisha ya watu, kushinda vita dhidi ya umasikini na kujitahidi kufikia lengo la kukamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote mwaka huu. China imeweka lengo la kutoa nafasi mpya za ajira mijini mwaka huu kuwa zaidi ya milioni 9, na kudhibiti kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kuwa karibu asilimia sita. Kutokana na hali tete iliyotokana na maambukizi ya COVID-19 na hali ya kiuchumi na kibiashara duniani, maendeleo ya China yanakabiliwa na sintofahamu kadhaa, hivyo serikali ya China haijaweka malengo maalum ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu. Ripoti hiyo pia imesisitiza kwamba China itaendelea na hatua ya kuzuia na kudhibiti virusi vya Corona katika kipindi kijacho, na kushughulikia vizuri maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

  Kuhusu kutumia vizuri uwekezaji wa nje na kufungua mlango zaidi, Bw. Li amesema,

  "China itapunguza zaidi orodha ya sekta zinazopiga marufuku uwekezaji kutoka nje, kuweka orodha ya sekta zinazopiga marufuku biashara ya huduma ya kuvuka mipaka, na kuyapatia maeneo ya majaribio ya biashara huria haki zaidi ya kujiamulia juu ya mageuzi na kufungua mlango. "

  Ameongeza kuwa China inalinda kithabiti mfumo wa biashara ya pande nyingi, na kushiriki kwenye mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani. Pia inahimiza kusaini makubaliano ya ushirikiano wa wenzi wa kiuchumi wa pande zote wa kikanda RCEP, kuhimiza mazungumzo ya biashara huria kati ya China, Japan na Korea Kusini, na kutekeleza kwa pamoja makubalilano ya kibiashara ya awamu ya kwanza kati ya China na Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako