• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasisitiza nia thabiti ya kulinda usalama wa taifa licha ya tishio la Marekani kuhusu Hong Kong

  (GMT+08:00) 2020-05-22 21:13:30

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema usalama wa taifa ni msingi wa kuwepo na maendeleo ya nchi moja, na hakuna nchi inayoruhusu vitendo vya kutenganisha taifa na kuharibu usalama wa taifa katika ardhi zake.

  Zhao amesema hayo baada ya rais Donald Trump wa Marekani kutishia kuweka vikwazo vikali dhidi ya mtu yeyote anayeharibu kujitawala kwa Hong Kong. Zhao amesema Hong Kong ni eneo lenye utawala maalum la China, na suala la serikali ya Hong Kong kutunga sheria kulinda usalama wa taifa ni mambo ya ndani ya China na nchi yoyote haitakiwi kuingilia.

  Zhao amesisitiza kuwa serikali ya China ina nia thabiti ya kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya taifa, kutekeleza sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" na kupinga nchi za nje kuingilia kati masuala ya Hong Kong.

  Muswada wa uamuzi wa kuanzisha na kuboresha mfumo wa kisheria na utekelezaji wa sheria kwa ajili ya Hong Kong ili kulinda usalama wa taifa umewasilishwa leo kwenye mkutano wa 3 wa Bunge la 13 la Umma la China NPC ili kujadiliwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako