• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Msomi wa Kenya asema China kutoweka lengo la ukuaji wa uchumi ni sahihi na ni uamuzi mwafaka

  (GMT+08:00) 2020-05-23 10:32:47

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa ripoti ya kazi ya serikali, ambayo inafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Msomi wa Kenya Bw. Stephen Ndegwa anaona kuwa kufunguliwa kwa mikutano miwili ya China ambayo ni mkutano wa bunge la umma na mkutano wa baraza la mashauriano ya kisiasa kumetia moyo mapambano ya kimataifa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani.

  Bw. Stephen Ndegwa ambaye ni mtaalamu wa sera za umma za Afrika wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani, na pia ni mtaalamu wa masuala ya China amesema, hatua ya China kutoweka lengo la ongezeko la pato la taifa katika mwaka mpya ni uamuzi sahihi unaoendana na hali halisi.

  Bw. Ndegwa amefafanua kuwa, kutokana na athari zinazotokana na maambukizi ya virusi vya Corona na biashara za kimataifa, uchumi wa kila nchi duniani unakabiliwa na matatizo, China pia inakabiliwa na hatari isiyoweza kukadiriwa. Aidha China imeweka malengo mengine katika utoaji wa nafasi za ajira, na kutangaza hatua za kupunguza kodi kwenye makampuni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako