• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China ashiriki kikao cha wajumbe wa sekta ya uchumi wa baraza la mashauriano ya kisiasa

  (GMT+08:00) 2020-05-23 14:48:28

  Rais Xi Jinping wa China amewatembelea wajumbe wa kikundi cha sekta ya uchumi waliokuja kwenye mkutano wa mwaka wa baraza la mashauriano ya kisiasa, ambapo amehudhuria kikao hicho na kusikiliza maoni na mapendekezo.

  Tangu kuanza kwa mkutano mkuu wa awamu ya 18 wa wajumbe wa chama cha kikomunisiti cha China, kila mwaka rais Xi anawatembelea wajumbe wa baraza la mashauriano ya kisisa, na kujadili mambo ya taifa. Hii ni mara yake ya kwanza kushiriki kikao cha wajumbe wa sekta ya uchumi, kinachojumuisha wakuu wa idara za uchumi za serikali kuu, wakuu wa makampuni makubwa yanayomilikiwa na taifa, wakuu wa mashirika ya kifedha na wachumi wengi maarufu. Wakati maendeleo ya uchumi na jamii ya China yakiathiriwa na maambukizi ya virusi vya Corona, kikao hicho kinachohudhuriwa na rais Xi kinafuatiliwa sana na watu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako