Timu ya uokozi imepata miili 97 kutoka kwenye mabaki ya ndege ya Shirika la ndege la Kimataifa la Pakistan PIA, iliyopata ajali jana kwenye eneo la makazi mjini Karachi. Kwenye taarifa yake jeshi la Pakistan limesema limepata watu wawili walionusurika na ajali. Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 91 na wafanyakazi wanane iliondoka uwanja wa ndege wa Iqbal huko Lahore mnamo saa 7:08 mchana na kuanguka saa 8:45 mchana. Ingawa ndege hiyo imepata ajali kwenye eneo la makazi lakini hakuna kifo kilichoripotiwa kwa watu waliokuwa chini, hata hivyo 17 wamepata majeraha kadhaa, na hali zao ni nzuri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |