• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Majaribio ya chanjo ya COVID-19 ya China yaonesha matokeo ya kutia moyo

  (GMT+08:00) 2020-05-23 18:05:21

  Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa jana kwenye mtandao wa jarida la kimatibabu The Lancet, majaribio ya chanjo ya COVID-19 ya China, ambayo ni chanjo ya kwanza kufikia hatua ya majaribio ya kliniki, imeonekana iko salama, inavumilika vizuri, na inaweza kutoa mwitikio wa kinga dhidi ya SARS-COV-2 kwa binadamu.

  Kwenye taarifa yake kwa wanahabari jarida hilo limesema majaribio ya wazi kwa watu wazima wenye afya 108 yameonesha matokeo yanayotia moyo baada ya siku 28, na matokeo ya mwisho yatatathminiwa baada ya miezi sita. Majaribio zaidi yanahitajika ili kuweza kubaini kama mwitikio wa kinga uliotolewa unalinda kwa ufanisi maambukizi ya SARS-VOV-2. Hata hivyo Profesa Chen Wei kutoka Taasisi ya Biotechnology ya Beijing, China ambaye ni kiongozi wa utafiti huo amesema matokeo haya yanapaswa kutafsiriwa kwa uangalifu, kwani changamoto za kukuza chanjo ya COVID-19 si za kawaida, na uwezo wa kuchochea mwitikio huu wa kinga sio lazima uwe unaonesha kwamba chanjo italinda watu dhidi ya COVID-19. Amesisitiza kuwa ingawa chanjo inatia moyo lakini bado ni mbali sana kwa chanjo hii kuweza kupatikana kwa watu wote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako