Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametoa shukurani za Wazimbabwe kwa timu ya wataalamu wa afya wa China kwa kutoa uzoefu na maarifa yao kwa wafanyakazi wa matibabu waliopo mstari wa mbele wa Zimbabwe katika kupambana na janga la COVID-19.
Rais Mnangagwa ameendelea kutoa shukurani zake kwenye barua iliyosomwa na waziri wa afya wa Zimbabwe Obadiah Moyo kwenye mkutano wa pamoja na wanahabari katika kuhitimisha ziara ya wiki mbili ya timu ya China nchini humo. Amesema wafanyakazi wa matibabu wa nchi hiyo wamenufaika sana na maarifa ya timu hiyo iliyo mstari wa mbele kupambana na COVID-19.
Katika ziara yao, timu hiyo yenye wataalamu wa afya 12 wa China walikwenda mikoa minne kati ya 10 nchini humo na kutoa uzoefu wao kwa wafanyakazi wa matibabu wanaopambanana na virusi vya corona. Timu hiyo pia imechangia vifaa tiba katika hospitali walizotembelea zikiwemo Hospitali ya Mkoa wa Marondera, Hospitali ya Mkoa wa Chinhoyi na Hospitali ya Mvurwi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |