• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kitendo chochote cha kujaribu kukosoa nia ya serikali kuu ya China kuilinda Hong Kong kitashindwa

    (GMT+08:00) 2020-05-24 10:50:29

    Mkutano wa tatu wa bunge la umma la awamu 13 umejadili mswada wa "Uamuzi wa bunge la umma la China kuhusu kuzindua na kukamilisha mfumo wa sheria na mfumo wa utekelezaji wa kulinda usalama wa taifa wa eneo la utawala maalum la Hong Kong." Hatua hiyo imeonesha kuwa jaribio lolote lenye nia ya kuleta changamoto kwa nia ya serikali kuu ya China kuilinda Hong Kong ya litashindwa.

    Bunge la umma la China kujadili mswada huo kunalenga kuilinda sera ya "Nchi Moja Mifumo Miwili", kulinda ustawi na utulivu wa Hong Kong na amani ya kudumu ya taifa na kukidhi matakwa ya maisha ya amani ya wakazi wa Hong Kong.

    Nguvu inayojaribu kuvuruga hali ya Hong Kong inadai kuwa sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong inakiuka haki za binadamu za wakazi wa eneo hilo. Hoja hiyo inalenga kuchafua sheria hiyo na kukusudia kusema uwongo. Bunge hilo linataka kuhimiza utungaji wa sheria wa Hong Kong katika upande wa kulinda usalama wa taifa, ambalo halilengi kutoa ufafanuzi mpya kwa mfumo wa jamii ya Hong Kong na haki za msingi za wakazi wa eneo hilo.

    Kinachotakiwa kusisitizwa ni kwamba jamii yenye ustaraabu haina haki isiyo na majukumu, wala haina uhuru usio na wajibu. Wakazi wa Hong Kong siku zote wana haki mbalimbali kwa kufuata sheria. Wakati huohuo, kulinda usalama wa taifa na kuhakikisha sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" ni wajibu wa wakazi wote wa Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako