• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanakijiji wa "Kijiji cha Mwamba" wahamia kwenye nyumba mpya

  (GMT+08:00) 2020-05-24 13:41:51

  Kijiji cha Atule'er kilichoko wilaya inayojitawala ya kabila la Yi ya Liangshan mkoani Sichuan, kusini magharibi mwa China, kinajulikana kama "Kijiji cha Mwamba", ambako wanakijiji inawabidi wapande mwamba wenye kimo cha mita 800 ili kwenda nje na kurudi nyumbani. Tatizo la usafiri ni sababu kuu inayopelekea umaskini wa kijiji hicho.

  Mwezi Julai mwaka 2016, serikali za huko zilitenga Yuan milioni moja, sawa na dola laki 1.4 za kimarekani kwa ajili ya kujenga ngazi ya chuma cha pua, ikifuatiwa na ujenzi wa miundombinu mingine, kama vile maji, umeme na huduma ya mtandao ilikuwa inapatikana. Mandhari ya kipekee ya kijiji hicho inawavutia watalii wengi kuitembelea. Kutokana na shughuli za utalii, pato la wastani la wanakijiji lilizidi dola 800 za kimarekani mwaka jana.

  Ili kuondoa tatizo la usafiri, serikali imeanza kutekeleza mradi wa uhamiaji kwa wanakijiji hao, ambao watu maskini wa familia 84 wamehama kwenye "mwamba" na kuhamia kwenye nyumba mpya wilayani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako