• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Kusini asema maendeleo ya uchumi wa China yatainufaisha dunia

    (GMT+08:00) 2020-05-24 13:42:25

    Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Kusini, ambacho ni taasisi inayofuatilia maendeleo na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea, Bw. Carlos Correa amesema, kufunguliwa kwa mkutano wa mwaka wa Bunge na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa nchini China ni ishara kwamba, nchi hiyo imepata mafanikio makubwa katika kudhibiti virusi vya Corona. Ufufukaji na maendeleo ya uchumi wa China vitasukuma mbele ufufukaji wa uchumi wa dunia.

    Amesema nchi nyingi za Afrika, Latin Amerika na Asia zinafanya biashara na China. Ufufukaji wa uchumi wa China utazinufaisha nchi hizo na dunia nzima, kwani utaleta kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa, kuchochea mambo ya biashara na kuongeza uwekezaji.

    Ameongeza kuwa China imepata mafanikio makubwa katika kuondoa umaskini, uzoefu wake unaweza kuigwa na nchi nyingi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako