• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkurugenzi wa Taasisi ya Virusi ya Wuhan athibitisha kuwa COVID-19 haikutokea kwenye maabara yake

  (GMT+08:00) 2020-05-24 17:10:22

  Mkurugenzi wa taasisi ya virusi ya Wuhan Bibi Wang Yanyi amesema suala la kutafuta chanzo cha virusi, ni suala la kisayansi linalowataka wanasayansi kufanya maamuzi kwa mujibu wa ushahidi.

  Akiongea kwenye mahojiano maalum na Televisheni ya China CGTN, Bibi Wang amesema uvumi kuwa virusi vya COVID-19 vilitoka kwenye maabara ya taasisi ya virusi ya Wuhan, si kweli.

  Amesema ni kweli taasisi ya virusi ya Wuhan inafanya utafiti wa virusi, na wao waligundua virusi vyenye kufanana na COVID-19 kwa asilimia 96.2. Kwa watu wasio wataalam, mfanano wa asilimia 96.2 unaweza kuonekana kama ni mkubwa sana, lakini kitaalamu itachukua muda mrefu sana kwa virusi hivyo kufanana na COVID-19.

  Pia amesema jumuiya ya wanaakademia ya kimataifa imefikia makubaliano kuwa virusi vilitoka kwa wanyama pori, lakini kuna wanyama wengi sana. Amesema ushirikiano wa wanasanyansi wote duniani ndio utakaoweza kuleta majibu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako