• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa mambo ya nje wa China asema kusaidiana ni matumaini ya pamoja ya watu wa China na Marekani

  (GMT+08:00) 2020-05-24 18:54:07

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo akizungumza na wanahabari amesema, janga la Corona ni adui wa pamoja wa China na Marekani, kuungana mkono na kusaidiana ni matumaini ya pamoja ya watu wa nchi hizi mbili.

  Bw. Wang amesema inasikitika kuona kuwa, pamoja na kuenea kwa virusi vya Corona, virusi vingine vya kisiasa vimesambaa nchini Marekani, ambavyo vinaishambulia na kuikashfu China kwa kutumia fursa yoyote. Ametoa wito kwa nchi hizo mbili zifanye mambo matatu: Kubadilishana uzoefu na kusaidiana katika kupambana na virusi vya Corona; Kuitikia mwito wa jumuiya ya kimataifa juu ya kushiriki na kuhimiza ushirikiano wa pande nyingi kwenye mapambano hayo; na Kufanya mazungumzo juu ya namna ya kupunguza athari mbaya kwa uchumi wa nchi mbili na wa dunia nzima. Ameongeza kuwa China na Marekani zenye mifumo tofauti ya kijamii na staarabu tofauti, zinapaswa kutafuta njia mwafaka ya kuishi pamoja kwa amani na kunufaishana.

  Bw. Wang amesema, kuna nguvu za kisiasa nchini Marekani ambazo zinataka kupelekea uhusiano wa nchi hiyo na China hadi vita vipya vya baridi. Alionya kwamba, hii ni hatari sana, ambayo itaharibu utulivu na ustawi wa dunia nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako