• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Hali yazidi kuwa tete kwenye klabu ya Barcelona

  (GMT+08:00) 2020-05-25 08:13:05

  Mwezi mmoja baada ya wanachama sita wa Bodi ya Usimamizi ya Barcelona kujiuzulu, hali inaendelea kuwa mbaya zaidi kambini mwa kikosi hicho cha Ligi Kuu ya soka ya Uhispania (La Liga). Hii ni baada ya baadhi ya wachezaji kumweleza kocha Quique Setien na Rais Josep Bartomeu Maria kwamba hawajaridhishwa kabisa na namna ambavyo klabu hiyo inaendeshwa. Miongoni mwa wachezaji hao ni beki Clement Lenglet, 24, ambaye amekiri kwamba ni wanasoka wachache sana kwa sasa wanaofahamu mustakabali wao kambini mwa Barcelona. Japo Lenglet ameridhisha zaidi kambini mwa Barcelona katika jumla ya mechi 29 zilizopita, amesisitiza kwamba atakuwa mwepesi zaidi wa kubanduka ugani Nou Camp iwapo ofa ya kuvutia zaidi itamjia. Kwa mujibu wa magazeti mengi nchini Uhispania, ni wachezaji Marc-Andre ter Stegen, Gerard Pique, Frenkie de Jong, Antoine Griezmann, Lionel Messi na Ansu Fati pekee ndio walio na mustakabali ulio na matumaini tele kambini mwa Barcelona. Mbali na Lenglet, wengine ambao wamefichua maazimio ya kuagana rasmi na Barcelona baada ya kulalamikia mazingira mabaya ya kufanyia kazi ni Ivan Rakitic, Arturo Vidal na Jean-Clair Todibo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako