• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jumuiya ya kimataifa yasema mikutano miwili ya kisiasa ya China itaimarisha imani ya dunia

  (GMT+08:00) 2020-05-25 09:29:41

  Mikutano mikuu miwili ya kisiasa nchini China ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China na Mkutano wa Bunge la Umma la China inayoendelea kufanyika, inafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa, ambayo inasema mikutano hiyo itaimarisha imani ya dunia.

  Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Ushauri kwa Uhusiano wa Wenzi wa Ushirikiano kati ya Kampuni za Kiserikali na Kibinafsi ya serikali ya Uingereza Bw. John Davie, amesema serikali ya China imezingatia vya kutosha athari ya mlipuko wa virusi vya Corona, na malengo yaliyowekwa na ripoti ya kazi za serikali ni wazi na yenye ufanisi. Anasema,

  "Naona malengo yaliyowekwa kwenye ripoti ya kazi za serikali ya China yatapiga hatua kubwa katika kuongeza matumizi ya ndani, ambapo yatahusisha suala la kuondoa umaskini. Kuongeza mahitaji ya ndani pia kunasaidia kuondoa umaskini. Hakuna kitu kingine kinachoweza kuboresha maisha ya watu zaidi kuliko utoaji wa kazi nzuri. Kuondoa umaskini kutaboresha maisha ya watu."

  Profesa Nadia Helmy wa Chuo Kikuu cha Beni-Suef cha Misri, ambaye pia ni mtaalam wa mambo ya China amesema anafuatilia sana hatua mbalimbali za kiuchumi zilizotajwa na ripoti ya kazi za serikali ya China, ambazo zimeonesha mawazo ya kiutawala ya China, na nia na jitihada zake za kufufua uchumi baada ya janga la virusi vya Corona.

  Mkurugenzi wa ofisi ya uchunguzi wa sera za China ya Hispania, ambaye pia ni mtaalam maarufu wa mambo ya China Bw. Xulio Rios amesema, mikutano hiyo miwili inafanyika wakati dunia inakabiliwa na janga la COVID-19, hivyo inafuatiliwa zaidi na jumuiya ya kimataifa. Ameongeza kuwa mwaka huu China haijataja lengo halisi la ukuaji wa uchumi, kutokana na sintofahamu zinazoletwa na janga la virusi vya Corona duniani, hata hivyo mwaka huu China itatimiza malengo ya kutokomeza umaskini unaokithiri na ujenzi wa jamii yenye maisha bora.

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika jana alasiri amesema, Afrika ni ndugu mkubwa wa China, na watu wa pande hizo mbili wameshirikiana bega kwa bega kupigania ukombozi na maendeleo. Naibu mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Mataifa Bw. Kwesi Quartey ameishukuru China na wananchi wake kwa kutoa misaada kwa Afrika katika muda mrefu uliopita, na kusema Afrika inathamini urafiki kati yake na China. Anasema,

  "China siku zote inaunga mkono Afrika. Ilifanya hivyo wakati tunatafuta ukombozi. Maendeleo ya China kwa njia ya amani yameipa Afrika uwezekano mwingine wa kujiendeleza, yaani mawazo sahihi ya kisiasa na uongozi bora. China pia imetupatia misaada mingi kupambana na COVID-19. Tunaishukuru sana. Aidha tunapaswa kushirikiana ili kuondoa kashfa mbalimbali kwa njia wazi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako