• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kigali wafanyiwa ukarabati

    (GMT+08:00) 2020-05-25 15:42:25
    Kusitishw akwa muda kwa safari zote za ndege nje na ndani ya Rwanda, kumetoa fursa kwa serikali ya Rwanda kufanyia marekebisho ya kiufundi uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kigali.

    Shirika la kusimamia viwanja wa ndege nchini Rwanda (RAC), linaendesha ukarabati huo ambao utaongeza nafasi za kuegesha ndege zaidi, kuongeza nafasi ya wageni wanaowasili na vile vile njia maalum ya ndege kupaa.

    Shirika la kusimamia viwanja vya ndege nchini huko linasema kwamba, zaidi ya dola milioni 30 zimetumika katika ukarabati na upanuzi wa uwanja huo wa ndege kwa miaka mitatu iliyopita.

    Kwa miaka mitatu mtawalia kuanzia 2014-2017, Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kigali ulikuwa miongoni mwa viwanja 10 bora vya ndege kote Afrika, kwa mujibu wa utafiti kulingana na maoni ya wasafiri.

    Tayari serikali kuu ya Rwanda imetangaza kuwa imetenga faranga bilioni 145 ili kusaidia shirika la ndege kujikwamua baada ya kusitiosha shughuli zake k utokana na janga la virusi vya corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako