• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Kiwanda cha chumvi chafunguliwa Uganda

    (GMT+08:00) 2020-05-25 15:43:42
    Kiwanda cha kutengeneza chumvi kimefunguliwa katika eneo la Lugazi, wilaya ya Buikwe. Kiwanda hiki kinatapunguza gharama ya taifa la uganda ya kuagiza chumvi kutoka mataifa ya nje.

    kaimu mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho cha kampala Salt, Bwana Alok Kala, anasema kwamba kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani 16,000 za chumvi .

    Vile vile, kiwanda hiki kwa sasa kimetoa ajira kwa watu 100 na kinatarajiwa kuongeza wengine 200 hivi karibuni.

    Kulingana na waziri wa Fedha katika sekta ya kibinafsi na uwekezaji Bi Evelyn Anite, taifa la Uganda liliagiza tani 177,178 za chumvi kwa kima cha dola milioni 25 mwaka uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako