• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mario Gotze kuagana rasmi na Dortmund mwishoni mwa msimu huu

    (GMT+08:00) 2020-05-25 17:09:25

    Nyota wa timu ya taifa ya Ujerumani, Mario Gotze, atamaliza rasmi mkataba kati yake na Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu wa 2019-20. Mkurugenzi wa Michezo kwenye klabu hiyo, Michael Zorc, amesema fowadi huyo anasakwa na klabu kadhaa maarufu za bara Ulaya zikiwemo Leicester City, Liverpool, Bayer Leverkusen na AC Milan. Hadi kufikia sasa, Gotze, 27, amecheza jumla ya mechi 201 na Borussia Dortmund japo amepangwa katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo katika jumla ya michuano mitano pekee ya Bundesliga msimu huu. Sogora huyo wa zamani wa Bayern Munich anajivunia ufanisi wa kunyanyua ubingwa wa taji la Bundesliga mara tano na ndiye aliyeifungia Ujerumani bao la ushindi dhidi ya Argentina na kuwanyakulia ufalme wa Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako