• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Chelsea wapanga kuachana na N'Golo Kante

  (GMT+08:00) 2020-05-25 17:10:28

  Uondozi wa timu ya Chelsea, umedai upo tayari kumruhusu kiungo wao N'Golo Kante kuikosa michezo yote iliyobaki ya msimu huu wa 2019-20 kama ataendelea kuwa na hofu ya kuenea kwa virusi vya corona. Wiki iliyopita, mchezaji huyo alijiunga na wachezaji wenzake katika maandalizi ya mazoezi ya pamoja mara baada ya kufanyiwa vipimo, lakini hakuweza kufanya mazoezi na kuomba kurudi nyumbani kutokana na hofu hiyo ya virusi vya corona. Mchezaji huyo raia wa nchini Ufaransa, amekuwa na matatizo ya kiafya siku za hivi karibuni ambapo alianguka mazoezini siku chache kabla ya ligi kusimama kutokana na kusumbuliwa na tatizo la moyo. Inasemekana kuwa, Chelsea wamedai wapo tayari kumuacha akapumzika hadi mwisho wa msimu huu kama bado ana hofu na corona hadi pale atakapokuwa sawa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako