• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Masumbwi kurejea Tanzania Julai

    (GMT+08:00) 2020-05-25 17:10:46

    Promota wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Ally Mwanzoa amesema ataandaa mapambano na la kwanza litafanyika Julai 7 mwaka huu. Promota huyo amesema, mapambano hayo yatakuwa ya ndani na sasa wanaangalia uwezekano wa kuanza kufanyika kati ya jijini Dar es Salaam au Tanga. Mbali na mapambano hayo ya Julai 7 lakini pia Agosti 8 huenda kukawa na pambano lingine litakalohusisha pia mabondia kutokana ndani na nje ya nchi. Amesema, sababu kubwa za mapambano hayo kuanza kufanyika Julai ni kuwapa mabondia muda wa zaidi ya mwezi mmoja wa maandalizi ya nguvu ili kurudi katika viwango vyao. Hata hivyo amesema kuwa, baada ya mapambano hayo, mwezi Desemba watafunga mwaka na mapambano ya usiku ya mabingwa ambayo yalitakiwa kufanyika miezi iliyopita lakini wakalazimika kuahirisha kutokana na uwepo wa virusi vya Corona (COVID-19) jambo lililopelekea Serikali ya Tanzania kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kusimamisha shughuli zote za michezo kwa zaidi ya miezi miwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako