• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vitendo vya wanasiasa wa nchi za magharibi vya kuidai China iwajibike na mlipuko wa virusi vya Corona havina msingi wowote

    (GMT+08:00) 2020-05-25 20:33:44

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amezungumza na waandishi wa habari kando ya Mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Umma la China, na kusema vitendo vya kudai China iwajibike na mlipuko wa virusi vya Corona havilingani na ukweli wa mambo na pia hayana msingi wa kisheria. Amesema China inapinga vikali lawama na madai ya kuitaka iwajibike na mlipuko wa virusi vya Corona yaliyotolewa na baadhi ya wanasiasa wa Marekani na nchi nyingine za magharibi.

    Kama Shirika la Afya Duniani WHO lilivyosema, virusi vinawezekana kutokea katika sehemu yoyote nchini China, na China vilevile ni mwathirika mbaya wa janga la mlipuko wa vurisi vya Corona. Kitendo cha kuitaka China iwajibike na janga hili, hakilingani na ukweli wa mambo, na pia kimekwenda kinyume maadili.

    Utafiti umeonesha kuwa, kesi za maambukizi ya virusi vya Corona zilitokea mwezi Novemba mwaka jana na hata mapema zaidi katika nchi za Marekani na Ufaransa, na wagonjwa hao hawakuwa wametoka nje ya nchi, ndiyo maana kuna uwezekano mkubwa kuwa virusi hivyo vililipuka katika sehemu nyingi duniani. Lakini kwanini wanasiasa wa Marekani wanailenga China?

    Katika suala la uwajibikaji, Marekani ndiyo nchi inayotakiwa kuwajibika na janga hilo. Baadhi ya wanasiasa wa Marekani walitoa taarifa zisizo za kweli kuhusu tarehe ya kulipuko wa janga hili nchini humo, na takwimu za vifo vya watu kutokana na janga hilo, na hivyo kuifanya Marekani kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu wenye virusi vya Corona waliovieneza katika nchi nyingine duniani.

    Kwa mujibu wa sheria ya kimataifa, vitendo na mali za taifa havisimamiwi na nchi nyingine, na kitendo cha Marekani cha kuidai China iwajibike na mlipuko wa virusi vya Corona, hakikubaliwi na kiasi kikubwa cha wataalamu na mashirika ya kimataifa. Baraza la chini la bunge la Ujerumani limetoa ripoti ikisema kuwa kitendo hicho cha Marekani hakina msingi wowote, kwani hakuna ushahidi unaothibitisha uhusiano kati ya mlipuko wa virusi vya Corona na kuathiriwa kwa Marekani.

    Vitendo hivyo vya Marekani kwa mara nyingine tena vimeonesha umwamba na vigezo viwili vya baadhi ya wanasiasa wa Marekani. Kama Bw. Wang Yi alivyosema: kitendo chochote kinachotaka kuvamia mamlaka na kudhuru heshima ya China kwa kisingizio cha kuishtaki, na kuharibu matokeo ya juhudi kubwa za watu wa China, kamwe hakitafua dafu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako