• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa bunge la umma la China aelezea upendo aliojionea akiwa mtu aliyejitolea kukabiliana na virusi vya Corona mjini Wuhan

    (GMT+08:00) 2020-05-26 09:55:51

    Bi. Yu Cheng kutoka shule nambari 2 ya viwanda vyepesi mjini Wuhan ni mjumbe wa bunge la umma la China. Katika majadiliano ya jopo la wajumbe walioshiriki kwenye mkutano wa tatu wa awamu ya 13 ya Bunge hilo yaliyofanyika hivi karibuni na kuhudhuriwa na rais Xi Jinping wa China, Bi. Yu alieleza shukrani zake kwa serikali na watu wa sekta mbalimbali kutokana na msaada wao mkubwa kwa mji wa Wuhan na mkoa wa Hubei.

    Wakati Wuhan ilipokuwa ikifungwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, Bi. Yu alikuwa mtu aliyejitolea, akiungana na wenzake na wafanyakazi wa serikali za mitaa kutoa huduma kwa wakazi wa eneo waliloshughulikia.

    Bi. Yu alisema watu wanne wa familia ya mfanyakazi mwenzake wote waliambukizwa virusi vya Corona kwa bahati mbaya. Familia yao nzima walishuhudia ugumu wa kushindwa kupata vitanda katika hospitali, na baada ya kulazwa katika hospitali ya muda iliyojengwa kwa ajili ya wagonjwa wenye dalili ndogo. Mume wa binti wa mfanyakazi wake alikuwa mgonjwa mahututi na alipelekwa katika wodi ya wagonjwa mahututi kwa wakati. Baadaye wao wanne wote walipona na kutoka hospitali. Binti wa mfanyakazi wake alimwandikia barua akisema baada ya kukumbuka mambo waliyopitia, anapenda kumshuruku rais Xi Jinping, kuwashukuru watu waliotoa msaada kwa mji wa Wuhan, na upendo walioonesha ataukumbuka maishani.

    Bi. Yu pia aliwahi kuongea na mzee mwenye umri wa miaka zaidi ya 80 aliyekuwa mgonjwa wa virusi vya Corona. Mzee huyo alimwambia Bi. Yu kuwa hajawahi kushuhudia janga baya la ugonjwa wa kuambukiza kama COVID-19, na ni vigumu kuamini kuwa China inaweza kudhibiti virusi hivyo ndani ya muda mfupi. Anaona ni chini ya uongozi wa chama cha kikomunisti cha China na mfumo wa ujamaa tu, mafanikio hayo yanaweza kupatikana.

    Wuhan ni mji ulio kando ya Mto Yangtze, na samaki ni mlo muhimu sana kwa maisha ya kila siku ya watu wa Wuhan. Bi. Yu alisema hawezi kusahau jinsi mzee Liao aliposhangaa kwa furaha tele alipopewa samaki hai.

    Rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara ya ukaguzi mjini Wuhan mapema mwezi Machi, alitoa wito wa kuhakikisha maisha ya wakazi ikiwemo upatikanaji wa mchele, mafuta ya kupikia, nyama, mayai n.k. Rais Xi pia alisema watu wa Wuhan wanapenda kula samaki, ni lazima kuwe na samaki wa kutosha.

    Kisha mji wa Wuhan uliunda idara maalum ya kushughukia utoaji wa vyakula vingine vya baharini, baada ya wafanyakazi wa eneo la makazi kukusanya oda za manunuzi ya wakazi, kampuni husika zilipeleka vyakula vya baharini nyumbani kwa wakazi zikishirikiana na watu waliojitolea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako