• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mchezaji wa Cameroon aaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo

    (GMT+08:00) 2020-05-26 16:29:55

    Ulimwengu wa soka bara Afrika unaomboleza kifo cha ghafla cha mchezaji soka wa Cameroon mwenye miaka 21, Joseph Bouasse ambaye aliaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo. Bouasse, ambaye alihamia Italia akitokea Cameroon akiwa na miaka 16, alikuwa mwingi wa matumaini ya kuimarisha taaluma yake alifariki Jumapili, Mei 24. Mzawa huyo wa Cameroon aliwakilisha timu ya akademia ya AS Roma kufuatia kufuzu kwake mwaka 2016. Hata hivyo, hakupata nafasi ya kuchezea timu ya kwanza, alikabithiwa nafasi ya kipekee kufanya mazoezi na Daniele De Rossi na Francesco Totti jijini Rome. Kabla ya kifo chake, Bouasse alikuwa mchezaji wa timu ya Romania, Universitatea Cluj ambapo alijiunga nao mnamo Februari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako