• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkusanyiko wa sheria za kiraia kuhimiza utawala wa China wenye sifa ya juu zaidi

    (GMT+08:00) 2020-05-26 16:55:56

    Katika mkutano wa Bunge la Umma la China na mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Taifa la China unaoendelea hapa Beijing, ukaguzi na mjadala kuhusu mswada wa mkusanyiko wa sheria za kiraia umekuwa moja kati ya ajenda zinazofuatiliwa zaidi. Endapo mswada huo utapitishwa, mkusanyiko huo wa sheria za kiraia utakuwa wa kwanza tangu Jamhuri ya Watu wa China kuanzishwa, na pia unasifiwa kama "ensaiklopidia ya maisha ya kijamii" na "azimio la kuhakikisha haki za kiraia".

    Mswada huo unaowasilishwa katika mkutano wa bunge la umma la China una vifungu saba na vipengele 1,260, na unahusisha sekta mbalimbali. Kutoka kuboresha haki ya kukodisha uendeshaji wa ardhi vijijini hadi kueleza kanuni za soko la makampuni, yote yemewekwa bayana katika mkusanyiko huo wa sheria za kiraia.

    Ukaguzi na mjadala kuhusu mswada huo unafanyika katika kipindi muhimu wakati China inapanga kutimiza kwa pande zote lengo la kujenga jamii yenye maisha bora, hivyo kupitishwa kwa mswada huo kutaisaidia China kutimiza lengo hilo. Mkusanyiko wa sheria za kiraia pia utakuwa alama ya China kuhimiza kwa pande zote kuitawala nchi kwa kufuata sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako