• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachambuzi wa Sudan waunga mkono hatua ya China ya kuboresha mfumo wa sheria mkoani Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-05-26 17:22:31

    Wachambuzi kutoka nchini Sudan wamekubaliana na haki halali ya China ya kuboresha mfumo wa sheria na utekelezaji wake katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, na kuhakikisha ulinzi wa mfumo wa kanuni ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili".

    Profesa Khalid Dirar wa kitivo cha sayansi ya siasa katika Kituo cha Mikakati ya Utafiti mjini Khartoum amesema, China ina haki ya kutekeleza sheria inayoona inafaa kuboresha utaratibu wa kisheria na mfumo wa utekelezaji. Amesisitiza umuhimu wa kudumisha kanuni ya "Nchi Moja Mifumo Miwili", akisema kanuni hii imeonyesha kufaa kupitia utekelezaji wake katika mikoa ya Hong Kong na Macau, na haitakiwi kupuuzwa.

    Mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Sudan Abdul-Raziq Ziyada amesema, uamuzi huo wa China umekuja katika wakati mwafaka, na kusisitiza tena kuwa nia thabiti ya serikali ya China kulinda usalama wa taifa na kuzuia vurugu katika utulivu wa mkoa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako