• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kisirani kimeingia kwenye dili la Mohamed Bin Salman kuinunua Newcastle United

    (GMT+08:00) 2020-05-27 08:33:20

    Hivi karibuni ku4mekuwa na jina kubwa la bilionea wa Saudi Arabia Mohamed Bin Salman kuwa yupo kwenye hatua za mwisho kuinunua klabu ya Newcastle United. Baada ya awali kuripotiwa kuafikiana dau la pound milioni 300 la kuuziana klabu hiyo kutoka kwa mmiliki, sasa imeripotiwa kuwa Bin Salman ameanza kupata vikwazo na anaweza kushindwa kuinunua klabu hiyo. Taasisi ya WTO (World Trade Organizations) imeripotiwa kuwa Mei 11 iliwasilisha waraka wenye kurasa 123 ambao unatajwa kuwa utawekwa hadharani Juni 16 ukieleza kupinga kwa Prince Mohamed Bin Salman kuuziwa timu hiyo sababu ya Saudi Arabia kuwa katika orodha ya nchi zinazoongoza kuonesha mechi za EPL kinyume na sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako